DAR ES SALAAM Skendo ya mjini iliyotapakaa mjini na kwenye mitandao ya kijamii inamgusa modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto akidaiwa kujichora ‘tatuu’ ya mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ishu iliyosababisha mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumporomoshea matusi.
Kuhusu sakata hilo, mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta akimtolea povu Zari juu ya mwanaye huyo. Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu alipoulizwa kuhusu sekeseke hilo la mwanaye, mama Mobeto alisema kuwa, hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.
Hivi karibuni Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar. Source Global Publishers