(+VIDEO) RUGE MUTAHABA AFUNGUKA UKWELI KUHUSU PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS



Moja kati ya Stories kubwa sana weekend hii ni pamoja na inayomuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda kuhusu kuvamia ofisi za Clouds Media Group akiwa na Askari wenye silaha kwa kilichosemekana kwamba alifanya vurugu kituoni hapo.
Vurugu ambazo hapo awali ilisemekana ni kumpiga mmoja kati ya watangazaji wa kituoni hapo afahamikae kama Soudy Brown kwa kosa la kutorusha kipindi ambacho hapo awali ilisemekana walikubaliana kukifanya kilichokuwa kikihusu kumchafua Askofu Josephat Gwajima.
Asubuhi ya leo Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ndugu Ruge Mutahaba alikuwepo LIVE kwenye Exclusive Interview na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, na ameweza kufunguka kila kitu kuhusiana na taarifa hizo.
Ruge Mutahaba amefunguka kwamba ni kweli Mh. Paul Makonda alivamia kituoni kwake akiwa na askari wenye silaha na kuweza kuhoji ni kwanii kipindi hiicho hakijarushwa, na baada ya hapo alichukua flash iliyokuwa na kipindi hicho na kuondoka nayo.
Kitendo ambacho kilitengeneza hofu kwa kila mtu na kusababisha story kuwa kubwa na kila mtu kuhoji venye ambavyo alijisikia kutokana na kitendo hicho cha mkuu wa mkoa.

       TAZAMA MAHOJIANO MAZIMA HAPA